Watu 40 wauwawa katika ghasia kati ya Wahindu na Waislamu
5 Machi 2020Zaidi watu 40 waliuliwa katika makabiliano kati ya Wahindu na Waislamu nchini India, wataalamu wa haki za binadamu wanasema huenda waislamu wakalazimika kutafuta makazi mapya katika maeneo yasio na idadi kubwa ya Wahindu kwa kuhofia kushambuliwa tena.
Makabiliano hayo kati ya waislamu na Wahindu ndio mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini India katika miongo kadha iliopita, na yalizuka baada ya mandamano ya miezi kadha ya kupinga kupitishwa kwa sheria ya uraia yenye utata.
Katika sheria hiyo, serikali ya India inataka kuwapa uraia wahamiaji wa dini ya Kihindu, Budha na wakristo wanaokimbia unyanyansaji kutoka mataifa ya Pakistan Afghanistan na Bangladesh. Hatahivyo sheria hiyo inayojulikana kama 'CAA' haiwajumuishi waislamu.
Tangu kupitishwa ,mnamo Desemba mwaka jana, waislamu wamekuwa wakiandamana wakitaka sheria hiyo iondolewe. Pia wakiwa na hofu ya kuachwa nje bila uraia katika usajili wa orodha ya raia unaoatarajiwa kufanywa nchini humo.
Shiririka la Thomson Reuters limesema Alhamisi kuwa maelfu ya watu hasa waislamu wako katika hatari ya kulazimika kuyahama makazi yao kutokana na ghasia hizo ambapo Wahindu walionekana wakiwashambulia Waislamu katika mji mkuu New Delhi. Mtalaam wa haki za binadamu Miloon Kothari amesema kuwa baada ya ghasia hizo, serikali ya waziri mkuu Narendra Modi huenda pia ikawatenga waislamu, kuwanyima huduma bora pamoja na makazi mazuri. Ameliambia shirika la Thomsom Reuters.
Mapema Alhamisi polisi walionekana wakipiga doria katika barabara za mtaa wa Shiv Vihar, Kaskazini mashariki mwa mji mkuu New Delhi ambapo mapambano makali zaidi yalitokea.
Jamii ya Waislamu yaendelea kutengwa
Watalaamu wa haki za binadamu wanasema kuwa baada ya ghasia ziliowalenga waislamu katika mji wa Mumbai mwaka 1992 na 1993 nchini humo, idadi kubwa ya waislamu walikimbilia katika maeneo ya jamii zenye waislamu peke kwa kuhofu kushambulliwa.
Darshani Mahadevia, profesa katika chuo kiku cha Ahmedabad ameeleza kuwa baada ya ghasia za mwaka 2002 katika Mji wa Ahmedabad, maelfu ya waislamu walilazimika kuhama kutoka miji idadi kubwa ya Wahindu na kwenda maeneo yasio miundombinu bora pamoja na kukosa makazi mazuri.
Mnamo Juma tatu wabunge nchini humo walipurukushiana bungeni baada ya vyama vya upinzani kumtaka waziri wa mambo ya ndani Amit Shah ajiuzulu kutokana na jinsi serikali ilivyojibu mandamano ya kupinga sheria hiyo na hata kusambabisha ghasia hizo.
Wabunge wa upinzani walionekana wakibeba mabango na kuimba kauli za kumtaka waziri huyo ambaye pia ni mkuu wa polisi, ajiuzulu.
Chama tawala cha waziri mkuu Narendra Modi cha Bharatiya Janata kimetetea sheria hiyo kikisema inalenga kulinda watu dini ndogo Kusini mwa bara la Asia lakini wanaharakati na wakosoajai wamesema sheria hiyo inawabagua waislamu na pia ni kinyume na katiba ya India ambayo haiendeshwi kwa msingi wa dini yoyote.
Vyanzo : AFPE/RTRE