Watano wauawa kwa risasi madini haramu Afrika Kusini
31 Julai 2023Matangazo
Polisi ilisema miili mitano inayoaminiwa kuwa ya wachimbaji haramu ilipatikana karibu na shimo la kuingia mgodini karibu na eneo la mabanda la Riverlea magharibi mwa Johannerburg.
Taarifa ya polisi imesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa makundi mawili hasimu ya wachimbaji haramu yalikuwa yanafyatuliana risasi katika eneo hilo.
Soma zaidi: Ta'azia: Askofu Mkuu Desmond Tutu, mwanaharakati asiyechoka
Kuondoka kwa Zuma, kutaleta mabadiliko Afrika Kusini?
Ikiwa na kiwango cha ukosefu wa ajira cha asilimia 32, Afrika Kusini ina maelfu ya wachimbaji haramu waliopewa jina la utani la "zama zamas", ambalo ni neno la Kizulu linalomaanisha "wale wanaojaribu."