1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Watu 10 wauawa katika shambulizi la bomu kusini mwa Lebanon

17 Agosti 2024

Watu wasiopungua 10 wameuawa akiwemo mwanamke mmoja na watoto wawili katika shambulio la anga kwenye jengo la makazi kusini mwa Lebanon. Haya yamesemwa leo na wizara ya afya nchini humo.

https://p.dw.com/p/4jZwg
Shambulizi la Israel katika kijiji cha Marjayoun kusini mwa Lebanon mnamo Agosti 16.2024
Shambulizi la Israel katika kijiji cha Marjayoun kusini mwa LebanonPicha: Marwan Naamani/ZUMA Press Wire/picture alliance

Jeshi la Israel limesema lilishambulia ghala la silaha la wanamgambo wa Hezbollah katika eneo la Nabataea, kwa dhamira ya kuondoa tishio katika maeneo mengine ya kusini mwa Lebanon.

Soma pia:Shambulio la Israel laua wapiganaji wawili wa Hezbollah kusini mwa Lebanon

Wakati huo huo, wizara ya afya ya Lebanon imesema kwamba hapo jana Ijumaa, takriban mtu mmoja aliuawa na mwengine kujeruhiwa katika shambulizi la Israel lililolenga kijiji cha Aitaroun kusini mwa Lebanon.

Soma pia:Shambulizi la Israel laua wapiganaji watano wa Hezbollah

Huku hayo yakijiri, kundi la Hezbollah linalofadhiliwa na Iran, limesema mpiganaji wake mmoja aliuawa, lakini halikusema ni lini au wapi.

Jeshi la Israel nalo limesema eneo lilipolenga huko Aitaroun ni la kijeshi ambapo kundi la Hezbollah linaendesha shughuli zake.