Watu 10 wauawa kwa bomu Sudan
22 Januari 2024Matangazo
Chanzo kimoja katika hospitali iliyopo mji wa Shendi uliopo kwenye jimbo la Mto Nile kimeliambia shirika la habari la AFP kwamba watu hao 10 walikufa baada ya basi walilokuwa wamepanda kukanyaga bomu siku ya Jumamosi (Januari 20).
Basi hilo lilikuwa likiwasafirisha abiria kutoka mashariki mwa jimbo la Al-Jazira kuelekea Shendi, umbali wa kilomita 180 kutoka Khartoum.
Hili linaaminika kuwa tukio la kwanza, tangu kuibuka kwa vita kati ya majenerali wawili, Abdel Fattah al-Burhan, ambaye ni mkuu wa jeshi la Sudan na aliyekuwa naibu wake, Mohammed Hamdan Daglo.
Pande hizo zote hazijazungumzia chochote juu ya tukio hilo.