Watu 13 wafa maji wakijaribu kwenda barani Ulaya
29 Oktoba 2024Kulingana na taarifa za maafisa wa Libya na kutoka kwenye shirika moja linalotoa misaada kwa wakimbizi, mtu mmoja ndiye aliyenusurika kwenye mkasa huo.
Shirika hilo la misaada la nchini Libya, Al-Abreen, limesema boti hiyo ilizama umbali wa kilomita 60 katika pwani ya mji wa Tobruk wa mashariki mwa Libya jana Jumatatu jioni.
Wahamiaji 11 wafa baharini, 60 hawajulikani waliko
Shirika hilo limesema mtu huyo aliokolewa pamoja na maiti zilizoopolewa. Idara ya kupambana na uhamiaji haramu huko Tobruk pia imethibitisha tukio hilo.
Katika miaka ya hivi karibuni, Libya limekuwa ni taifa linaloongoza kuwa ni sehemu wanayoitumia wahamiaji wanaokimbia vita na umaskini kutoka barani Afrika na katika nchi za Mashariki ya Kati wanaojaribu kwenda barani Ulaya.