Watu 15 wameuliwa na polisi Kenya, wakati wa utekelezaji wa amri ya kutotembea usiku ili kuzuwia kusambaa kwa virusi vya corona viliyodumu kwa miezi miwili sasa. Mamlaka ya usimamizi wa polisi IPOA, imesema inachunguza visa vingine 87 vya polisi kutumia nguvu kupindukia.