1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Watu 18 wauwawa katika shambulio la kigaidi Somalia

Angela Mdungu
15 Septemba 2024

Watu wasiopungua 18 wameuwawa baada ya bomu kulipuka katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, baada ya wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu wa Al shabaab kuyalipua mabomu mawili kwenye wilaya ya Kahda.

https://p.dw.com/p/4kdgE
Wanamgambo wa Al-Shabaab wamekuwa wakifanya mashambulizi mara kwa mara Mogadishu
Uharibifu uliotokana na moja ya mashambulizi ya kundi la Al-shabaab mjini MogadishuPicha: Hassan Ali Elmi/AFP via Getty Images

Afisa wa Polisi Mohamed Dahir amesema mabomu hayo yalifichwa kwenye sehemu maarufu ya mtaa mmoja kwenye eneo hilo na kuwa mlipuko ulitokea wakati, kundi la vijana wadogo walipokuwa wakipiga picha.

Watu 10 wamejeruhiwa kutokana na tukio hilo. Licha ya kundi la wanamgambo wa Al Shabaab kuondolewa mbali na Mogadishu, bado wanadhibiti sehemu kubwa ya Somalia.

Soma zaidi: Watu 11 wauawa katika shambulizi la kigaidi Mogadishu

Hivi karibuni watu 10 waliuwawa baada ya gari kulipuliwa kwa bomu mjini Mogadishu, wakati watu wengine 11 waliuliwa katika shambulio la kigaidi katika mgahawa mmoja wa mji huo mkuu katikati mwa mwezi Agosti.