1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 1,800 tu wasalia Avdiivka Ukraine

10 Aprili 2023

Vita vinavyoendelea sasa nchini Ukraine vimesababisha kupungua kwa idadi ya wakaazi wa mji wa Avdiivka kutoka 32,000 kabla ya vita hadi 1,800 hivi sasa,

https://p.dw.com/p/4Psbc
Ukraine Avdiivka
Picha: Genya Savilov/AFP/Getty Images

Vita vinavyoendelea sasa nchini Ukraine vimesababisha kupungua kwa idadi ya wakaazi wa mji wa Avdiivka kutoka 32,000 kabla ya vita hadi 1,800 hivi sasa, huku vikosi vya Urusi vikiendelea na jitihada za kutaka kuuteka mji huo.

Gavana  jimbo la Donetsk, Pavlo Kyrylenko, amesema Urusi imeugeuza mji huo kuwa magofu. Amesema mji huo ulishambuliwa na mashambulizi ya anga leo hii na kuporomosha jengo la ghorofa kadhaa.

Avdiivka umekuwa ukilengwa katika mashambulizi ya vikosi vya Urusi katika kipindi cha msimu wa baridi. Moscow ilitumaini kuudhibiti mji huo tangu Februari 2022, baada ya uvamizi wake ambao unaelezwa kuwa na mafanikio madogo katika eneo la mashariki.

Katika taarifa tofauti, Mkuu wa Majeshi wa Ukraine amesema vikosi vya Urusi vimekuwa vikiendelea na mashambulizi katrika maeneo yanaizunguka Avdiivka, lakini wanapoteza nguvu kubwa ya wapiganaji na vifaa.