1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiEthiopia

Watu 19 wapoteza maisha katika ajali ya boti nchini Ethiopia

29 Julai 2024

Takriban watu 19 wamepoteza maisha wakati boti iliyowabeba ilipozama kwenye mto Tekeze nchini Ethiopia. Shirika la habari katika eneo hilo AMC, limeripoti kwamba watu wazima sita na mtoto mmoja waliokolewa.

https://p.dw.com/p/4iq0O
Mwanajeshi wa Sudan ashika doria katika fuo ya mto Tekeze ulioko katika mpaka kati ya Sudan na Ethiopia baada ya vikosi vya Ethiopia kuwazuia watu kuvuka mto huo kuingia Sudan mnamo Desemba 3, 2020
Mto Teekeze nchini ulioko katika mpaka kati ya Sudan na EthiopiaPicha: Nariman El-Mofty/AP Photo/picture alliance

Boti hiyo ilikuwa ikiwavusha abiria kwenye mto huo, unaopita katika mpaka kati ya Ethiopia na Eritrea kuelekea Sudan na ilipata ajali hiyo katika makutano ya nchi hizo tatu. Maafisa wamekadiria kuwa watu wapatao 26 walikuwamo ndani ya boti hiyo wakati wa ajali hiyo ilipotokea majira ya mchana hapo jana.

AMC imeripoti kuwa ni miili miwili pekee iliyopatikana hadi sasa na kuongeza kuwa wale waliookolewa walipelekwa katika hospitali za karibu.

Ni vigumu kupata habari kwa haraka katika maeneo ya mbali ya kaskazini mwaEthiopia kutokana na udhibiti mkali wa serikali ambapo mara nyingi taarifa hupatikana baada ya muda mrefu tangu linapotokea jambo.