Watu 190 wamenusurika kwa ajali ya ndege nchini Uturuki
9 Mei 2024Kampuni yenye uratibu wa safari wa ndege hiyo aina ya Boing 737-800 ya shirika la ndege la Corendon la hukohuko Uturuki, imesema pamoja na tatizo hilo ndege ilifanikiwa kusimama uwanjani.
Ndege, ilikuwa na abiria 184 na wafanyakazi sita, ikitokea Cologne, Ujerumani. Shirika Corendon limekanusha ripoti za vyombo vya habari vya Uturuki kuwa ndege hiyo ilikuwa ikitua kwa kutanguliza eneo la mbele, yaani pua yake.
Soma pia: Polisi ya Uturuki yawatia mbaroni waandamanaji 200
Katika tukio lingine la jana Jumatano ndege ya mizigo ya Boeing 767 mali ya kampuni ya kusafirisha mizigo ya FedEx Express ilitua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul baada ya gia kushindwa kufanya kazi. Na kadhalika katika mkasa huo hakuna aliyejeruhiwa na wahudumu waliweza kufanya uokozi wa ndege hiyo salama.