Watu 21 wauawa kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi Msumbiji
25 Desemba 2024Waziri wa mambo ya ndani Pascoal Ronda amewaambia waandishi wa habari jana jioni kwamba jumla ya matukio 236 ya vurugu yaliripotiwa kote nchini humo na kusababisha majeruhi ya watu 25 wakiwemo maafisa 13 wa polisi.
Ronda amesema makundi ya watu wenye silaha wameshambulia vituo vya polisi, magereza na miundombinu mengine na kwamba hadi sasa zaidi ya watu 70 wamekamatwa.
Soma pia: Baraza la katiba laidhinisha matokeo ya uchaguzi Msumbiji
Waandishi wa shirika la habari la AFP wameripoti kuwa, mji mkuu wa Maputo uliokuwa na watu wachache hapo awali ulishuhudia makabiliano kati ya waandamanaji na polisi.
Mahakama ya juu kabisa ya taifa hilo ilithibitisha siku ya Jumatatu kwamba chama cha Frelimo kilichoko madarakani tangu mwaka 1975 kilishinda uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 9.