1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiHaiti

Watu 24 wamekufa baada ya lori la mafuta kulipuka Haiti

Angela Mdungu
15 Septemba 2024

Watu 24 wamefariki dunia baada ya lori la mafuta kulipuka karibu na mji wa Pwani wa Miragoane nchini Haiti. Tenki la lori hilo lilipasuka baada ya kugongwa na gari jingine na watu kukimbilia eneo la tukio kukinga mafuta.

https://p.dw.com/p/4kdg0
Lori la mafuta limelipuka na kusababisha vifo vya watu 24 Haiti
Mhudumu wa afya akimhudumia majeruhi wa ajali ya moto iliyotokana na Lori la mafuta kulipuka Haiti, 14.12.2021Picha: Ralph Tedy Erol/REUTERS

Taarifa iliyotolewa na serikali imebainisha kwamba watu 40 wamepata majeraha makubwa na wengine 15 wana majeraha madogo madogo.

Uingizaji wa mafuta katika eneo la Miragoane umepungua katika wiki za hivi karibuni kwa kuwa malori yamekuwa yakitumia njia ya kivuko ili kuepuka makundi ya wahalifu yanayodhibiti barabara kuu zinazouzunguka mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince.

Kusambaa kwa makundi hayo kulikochochea mgogoro mkubwa wa kiutu sasa kumesababisha taifa hilo litangaze hali ya hatari.