Watu 56 wafariki katika ajali ya ndege Uturuki
30 Novemba 2007Matangazo
Ajali ya ndege iliyotokea nchini Uturuki asubuhi ya leo,imeua abiria na watumishi wote wa ndege hiyo aina ya McDonell Douglas MD-83.Ndege ya shirika la AtlasJet iliyotoka Istanbul na kuelekea Isparta,ilikuwa na jumla ya watu 56. Ndege hiyo ilianguka sehemu za milimani na kwa hivi sasa,sababu ya ajali bado haijulikani.