Watu waliokamtwa Berlin sio washukiwa wanaotafutwa wa RAF
3 Machi 2024Matangazo
Kulingana na msemaji wa Polisi katika Jimbo la Saxony, Ulrike Trumtar, polisi walifanya msako katika mji wa Berlin mapema leo Jumapili wakiwasaka washukiwa hao kwa madai ya ugaidi na wamekuwa mafichoni kwa miongo kadhaa iliyopita.
Milio ya risasi ilisikika katika eneo la tukio lakini hakuna majeruhi walioripotiwa. Polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini iwapo watu wawili waliokamatwa leo wana uhusiano na kundi la RAF.
Katika miaka ya 1970 na 1980, RAF ilifanya mfululizo wa mashambulizi Ujerumani Magharibi wakati huo kupitia mashambulizi na utekaji nyara, huku jumla ya mauaji zaidi ya 30 yakihusishwa na kundi hilo.
Hata hivyo RAF ilisambaratishwa mnamo1998 na hakuna ushahidi kwamba kundi hilo la zamani la kigaidi bado linafanya kazi.