Watu wasiopungua 25 wamekufa ajali ya boti DR Kongo
18 Desemba 2024Matangazo
Taarifa hizo zimetolewa na maafisa wa serikali na wakaazi karibu mkasa huo ulipotokea. Imeelezwa chombo hicho kilikuwa kimewabeba zaidi ya abiria 100 kilipong´oa nanga kutoka mji wa Inongo, unaokutikana upande wa kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Kongo, Kinshasa.
Kilizama mita chache kutoka eneo kilipoanza safari ndani ya mto Fimi na watu wengine wengi bado hawajapatikana. Sughuli za uokoaji zinaendelea huku kukiwa na wasiwasi kwamba idadi ya waliopoteza maisha huenda itaongezeka.
Ajali hiyo ni ya nne ndani ya mwaka huu kwenye jimbo la Mai-Ndombe, ambalo limezungukwa na mito mingi na watu hutegemea kwa sehemu kubwa usafiri wa majini