1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhamiajiUfaransa

Watu karibu wanane wafa wakivuka ujia wa English Channel

16 Septemba 2024

Watu wasiopungua wanane wamekufa walipokuwa wakijaribu kuvuka ujia wa bahari wa English Channel kuingia Uingereza, zimesema mamlaka za usafiri wa majini za Ufaransa usiku wa Jumapili.

https://p.dw.com/p/4keJE
Uhamiaji | Ufaransa
Wazima moto na walinzi wa raia wakiwa wamechukua miili ya wahamiaji waliokufa baada ya boti yao kuzama walipojaribu kuvuka English Channel Septemba 3, 2024Picha: Denis Charlet/AFP

Mkasa huo ulitokea siku ya Jumamosi muda mfupi kabla ya majira ya saa sita usiku, wakati mamlaka hizo zilipogundua boti iliyokuwa imebeba watu kadhaa ikihangaishwa karibu na ufuo wa bahari kaskazini mwa nchi hiyo.

Mamlaka hiyo inayohusika na ujia huo imesema walipeleka meli ya uokozi ya Ufaransa kwenye eneo hilo, lakini watu wanane walikufa. Imesema hakukua na watu waliookolewa walipokuwa wakitafuta manusura.

Watu sita walipelekwa hospitalini "kutokana na hali mbaya," ikiwa ni pamoja na mtoto wa miezi 10 aambaye joto lake la mwili lilikuwa limeshuka sana ama "hypothermia."

Jacques Billant, Pas-de-Mkuu wa mkoa wa Calais, aliviambia vyombo vya habari vya Ufaransa jana Jumapili kwamba walionusurika
walitokea Eritrea, Sudan, Syria, Afghanistan, Misri na Iran.