1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Wawili wafa kwenye uvunjwaji wa madrasa India

9 Februari 2024

Watu wawili wameuawa nchini India na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika makabiliano ya kidini yaliyosababishwa na kuvunjwa kwa madrasa, katika muendelezo wa bomoabomoa inayoyalenga majengo ya Kiislamu nchini humo.

https://p.dw.com/p/4cDGC
Maafisa usalama wa India mjini Kolkata
Maafisa usalama wa India kwenye eneo la mzozo mjini Kolkata.Picha: Subrata Goswami/DW

Maafisa wa manispaa katika jimbo la kaskazini la Uttarakhand walivunja majengo ya madrasa siku ya Alkhamis (Februari 8) wakidai kwamba yalijengwa bila kibali.

Polisi imesema waandamanaji Waislamu waliwarushia mawe wakati wa maandamano yaliofuatia uvunjaji huo, na wakajibu kwa kufyatua gesi ya kutoa machozi.

Soma zaidi: Wahindu washambuliana na Wakristo India

Mamlaka katika mji wa Halswani ilisitisha huduma za intaneti, kufunga shule, kutangaza marufuku ya kutembea nje na kupiga marufuku mikusanyiko mikubwa baada ya kuzuka vurugu hizo.

Hekalu jipya la mungu Ram, lafichua mpasuko India

Makundi ya siasa kali ya Wahindu yamepata nguvu katika kampeni yao dhidi ya majengo ya Waislamu tangu Waziri Mkuu Narendra Modi alipoingia madarakani muongo mmoja uliopita.

Mwezi uliopita, Modi alizindua hekalu jipya la Kihindu katika mji wa kaskazini wa Ayódhya, lililojengwa kwenye eneo la msikiti wa karne kadhaa, ulioharibiwa na wanazi wa Kihindu mwaka 1992.