SiasaAsia
Waziri mkuu mpya Pakistan aapishwa
14 Agosti 2023Matangazo
Anwaar ul-Haq Kakar ameapishwa leo kuwa waziri mkuu wa mpito nchini Pakistan atakayesimamia mchakato wa uchaguzi mkuu wakati nchi hiyo ikiwa inakabiliwa na mkwamo mkubwa wa kisiasa na kiuchumi. Kakar ameahidi kuilinda katiba ya nchi wakati akiapishwa na rais Arif Alvi katika sherehe iliyofanyika ofisi ya rais.Mwanasiasa huyo hana umaarufu mkubwa ingawa inaaminika yuko karibu na jeshi akitokea chama cha Awami cha Balochistan ambacho kinatazamwa kama chama kilichoko karibu zaidi na jeshi lenye usemi mkubwa katika maamuzi ya kitaifa.