1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu Sunak kuongoza mikutano ya Akili Bandia

2 Novemba 2023

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak atakutana mjini London katika mkutano wa kilele wa teknolojia ya Akili bandia, na wawikilishi kutoka Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/4YKUB
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak Picha: Kin Cheung/REUTERS

Mkutano wao utajadili hatua zinazohitajika ili kuifanya teknolojia hiyo kuwa salama.

Haya yanajiri siku moja baada ya Sunak kupata uungwaji mkono wa China katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na athari za teknolojia hiyo.

Mkutano wa kujadili teknolojia ya akili bandia kufanyika Uingereza

Waziri Mkuu huyo atafanya vikao viwili, cha kwanza na nchi zenye mawazo sawa kuhusiana na suala hilo la akili bunifu na baada ya hapo atafanya kikao kingine na makampuni kama Google, Microsoft, Meta na xAI.

Afisi ya Sunak imesema yatakayojadiliwa ni mipango ya majaribio itakayoungwa mkono na mataifa husika na ukaguzi wa mitindo ya akili bunifu kabla haijatolewa.

Baadae atakuwa na mazungumzo na bilionea ambaye ni mmilki wa kampuni ya X Elon Musk.