1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Estonia asema hatonyamazishwa na Urusi

13 Februari 2024

Waziri Mkuu wa Estonia Kaja Kallas amesema hii leo kwamba kamwe hatonyamazishwa na ataendelea kuiunga mkono Ukraine bila kuyumba, licha ya Urusi kumworodhesha kuwa miongoni mwa watu inaowatafuta.

https://p.dw.com/p/4cM97
Waziri Mkuu wa Estonia Estlands Kaja Kallas akiwa Vienna
Waziri mkuu wa Estonia Kaja KallasPicha: Askin Kıyagan/Anadolu/picture alliance

Mapema hii leo Moscow ilitangaza kuwa imemweka kiongozi huyo wa Estonia pamoja na maafisa wengine wa mataifa ya Baltiki katika orodha ya watu inaowatafuta,  kuhusiana na madai ya kushiriki kuharibu makaburi ya mashujaa wa vita wa enzi ya dola ya kisovieti.

Mataifa matatu ya Baltiki ya Estonia, Latvia na Lithuania yaliyokuwa sehemu ya Muungano wa Kisovieti yamekuwa yakizivunja baadhi ya alama na minara ya kumbukumbu tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mwaka 2022. Urusi imeghadhibishwa na hatua hizo na imeapa kwamba waliohusika kuhujumu "alama za kumbukumbu za wakombozi wa ulimwengu dhidi ya Ufashisti na Unazi watawajibishwa."

Akijibu tangazo hilo, Kallas amesema Kremlin inatumai hatua hiyo itasaidia kumnyamazisha yeye pamoja na wengine lakini hilo halitatokea.