1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

India yataka kumalizika kwa vita kati ya Urusi na Ukraine

22 Oktoba 2024

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ametolea mwito wa kupatikana kwa suluhisho la vita vya Urusi na Ukraine, Modi ameyasema hayo katika mkutano wa kilele wa kundi la nchi zinazoinukia kiuchumi, (BRICS) huko Kazan, Urusi.

https://p.dw.com/p/4m6MH
Urusi BRICS I Rais Putin anampokea Waziri Mkuu wa India Modi huko Kazan
Rais wa Urusi Vladimir Putin akimkumbatia Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wakati wa mkutano wao kando ya Mkutano wa Wakuu wa BRICS huko Kazan, Urusi Oktoba 22, 2024.Picha: Alexander Zemlianichenko/Pool via REUTERS

Zaidi amesema "Mheshimiwa, tunawasiliana mara kwa mara kuhusu mzozo unaoendelea kati ya Urusi na Ukraine. Kama nilivyosema hapo awali, tunaamini kwamba matatizo yanapaswa kutatuliwa kwa amani, na tunaunga mkono kikamilifu uanzishwaji wa haraka wa amani na utulivu. Katika juhudi zetu zote, tunatoa kipaumbele kwa ubinadamu. Na tuko tayari kutoa msaada wowote unaowezekana katika siku zijazo." Putin hapo awali alimkaribisha Modi kwa bashasha na kumsifu kwa mahusiano mazuri baina ya nchi hizo mbili. Viongozi wengine wakuu wa nchi na serikali wamesafiri kwenda Urusi kushiriki mkutano huo. Kwa upande mwingine, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema anaitazama Urusi kama "mshirika wa thamani" na rafiki wakati wa mazungumzo na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin.