SiasaSenegal
Waziri Mkuu wa Senegal atangaza serikali yake mpya
6 Aprili 2024Matangazo
Sonko amesema rais Bassirou Diomaye Faye aliyeapishwa siku ya Jumanne kuiongoza Senegal baada ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa rais wa Machi 24, amewaidhinisha mawaziri wote waliopendekezwa.
Utendaji wa Baraza hilo jipya la mawaziri utafuatiliwa kwa karibu hasa kutokana na ahadi kubwa za mageuzi zilizotolewa na rais Faye wakati wa kampeni. Miongoni mwa hizo ni kuzifanyia ukaguzi mkubwa sekta za nishati ya mafuta, gesi pamoja na uchimbaji madini.
Miongoni mwa walioteuliwa kuwa mawaziri ni Cheikh Diba atakayeongoza wizara ya fedha na Abdourahmane Sarr atakuwa waziri wa uchumi. Majenerali wawili wameteuliwa kuongoza wizara ya mambo ya ndani na ya Ulinzi.