1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Rishi Sunak kutangaza msaada kwa Ukraine

21 Juni 2023

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak leo anatarajiwa kutangaza msaada mkubwa wa kifedha kwa Ukraine katika siku ya kwanza ya mkutano wa kimataifa unaonuwia kutafuta uungaji mkono wa kuijenga upya nchi hiyo

https://p.dw.com/p/4Ss5H
UK Rishi Sunak  in Nordirland
Picha: Liam McBurney/AP/picture alliance

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak hii leo anatarajiwa kutangaza msaada mkubwa wa kifedha kwa Ukraine katika siku ya kwanza ya mkutano wa kimataifa unaonuwia kutafuta uungaji mkono wa kuijenga upya nchi hiyo baada ya vita.  Mwanzoni mwa mkutano huo wa siku mbili unaofanyika mjini London, Sunak ataweka wazi kiwango cha msaada cha Uingereza ikiwemo kitita cha dola milioni 306 pamoja na dhamira ya kutanua uwekezaji wake nchini Ukraine.

Uingereza kuiwekea Ukraine dhamana ya mkopo

Vilevile Uingereza inataka kuiwekea dhamana Ukraine yenye thamani ya dola bilioni 3 ili taifa hilo lipatiwe mkono na Benki ya Dunia kutekeleza mipango ya kujijenga tena baada ya uharibifu uliotokana na vita. Uingereza imekuwa miongoni mwa wafadhili wakubwa wa Ukraine tangu Urusi ilipoivamia nchi hiyo mapema mwaka jana. Waziri Mkuu Sunak anatumai mkutano huo utaichochea sekta binafsi katika kuijenga upya Ukraine.