SiasaAsia
Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan afikishwa tena mahakamani
12 Mei 2023Matangazo
Uamuzi huo unaiweka serikali ya nchi hiyo na wafuasi wa kiongozi huyo katika nafasi ngumu baada ya siku kadhaa za kushuhudiwa makabiliano. Kikao cha leo cha mahakama ni sehemu ya mchakato mrefu wa kisheria. Jana Alhamisi mahakama ya juu kabisa ya nchi hiyo ilitowa uamuzi ikisema kwamba kukamatwa kwa Imran Khan kilikuwa kitendo kilichokwenda kinyume na sheria lakini ikaitaka mahakama ya juu ya Islamabad kutafakari uamuzi wake wa mwanzo wa kuunga mkono kukamatwa huko kwa Khan. Mahakama ya juu pia imesema itaheshimu uamuzi utakaochukuliwa leo na mahakama kuu ya Islamabad. Kwa upande mwingine serikali imesema itamkamata kiongozi huyo haraka ikiwa mahakama kuu ya Islamabad itamnyima dhamana ya kuachiliwa.