1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Imran Khan ahukumiwa miaka mitatu jela

5 Agosti 2023

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya Mahakama kumkuta na hatia katika kesi iliyokuwa inamkabili ya kupokea rushwa alipokuwa madarakani.

https://p.dw.com/p/4Uo74
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran KhanPicha: Akhtar Soomro/REUTERS

Kulingana na televisheni ya taifa ya nchini humo, Jaji Humayun Dilawar akitoa hukumu hiyo alisema madai ya kuhusika kwa Khan katika vitendo vya rushwa yamethibitishwa. Waziri mkuu huyo wa zamani wa Pakistan alikuwa akituhumiwa kwa kutumia vibaya madaraka yake kwa kuuza zawadi za nchi alizozipokea wakati wa ziara zake nje ya nchi.

Soma zaidi: Pakistan: Waziri mkuu wa zamani Imran Khan awekezwa kizuizi cha kusafiri nje ya nchi

Zawadi hizo zilikuwa na thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 635,000. Jeshi la polisi tayari limekwisha kumkamata Khan aliyekuwa mjini Lahore wakati hukumu yake ilipokuwa ikisomwa katika mahakama kuu ya mjini Islamabad.

Licha ya hukumu hiyo, mawakili wanaomtetea Khan wamesema kuwa watakata rufaa haraka. Ni pigo kwa Imran Khan aliyeazimia kurejea mamlakani kwa sababu hukumu hiyo inaweza kumzuia kushiriki kwenye maswala ya siasa.