1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nawaz Sharif kushiriki uchaguzi wa wiki hii Pakistan

5 Februari 2024

Nawaz Sharif, aliyewahi kuwa waziri mkuu mara tatu nchini Pakistan atashiriki uchaguzi mkuu siku ya Alhamisi akiwania nafasi hiyo kwa mara nyingine. Aliwahi kuhukumiwa kwenda jela miaka 10 mnamo mwaka 2018.

https://p.dw.com/p/4c2oC
Pakistan | Nawaz Sharif
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz SharifPicha: Ali Kaifee/DW

Nawaz Sharrif, aliyewahi kuwa waziri mkuu mara tatu nchini Pakistanatashiriki uchaguzi mkuu siku ya Alhamisi akiwania nafasi hiyo kwa mara nyingine.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 74 ambaye wafuasi wake wanamuita simba wa Punjab anakiongoza chama chake cha Pakistan Muslim League-Nawaz-(PML-N) kupata ushindi kwenye kinya'ng'anyiro hicho katika taifa hilo lenye wakaazi milioni 240 na lenye nguvu za Kinyuklia.

Aliwahi kuhukumiwa kwenda jela miaka 10 mnamo mwaka 2018,wiki tatu kabla ya uchaguzi, baada ya kushtakiwa kwa makosa ya ufisadi na kuzuiliwa kushikilia nafasi yoyote ya umma.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW