Ujerumani yatoa tahadhari kwa mvutano wa NATO na Urusi
1 Desemba 2024Akihojiwa na gazeti la Ujerumani la Handelsblatt lililochapishwa leo Jumapili, amesema tangu Urusi ilipoanzisha vita dhidi ya Ukraine,Ujerumani imeshuhudia kubadiliika kwa hali ya usalama wa ndani. Amesema Urusi inaendesha vita vya ndani barani Ulaya lakini akatowa mwito wa kujizuia kwa mataifa ya Ulaya akisema anatumai mstari wa jumuiya ya NATO hautovukwa. Waziri huyo wa mambo ya ndani wa Ujerumani amebaini kwamba rais Vladmir Putin amekuwa akionesha msimamo wa uchokozi zaidi kuelekea nchi kama Ujerumani ambayo ni mwanachama wa NATO,tangu ilipovamia Ukraine Februari 2022. Amesema mamlaka Ujerumani zitachukua hatua stahiki kukabiliana na hatua yoyote ya kuingilia uchaguzi wake ujao wa mapema na shirika la upelelezi wa ndani limeshaweka kikosi kazi.