1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Mambo ya Nje Fischer aufungua mkutano wa Munich

7 Februari 2004
https://p.dw.com/p/CFh2
MUNICH: Chini ya hatua kali za usalama mjini Munich ulifunguliwa mkutano wa 40 wa Kimataifa wa Usalama. Mnamo siku mbili zijazo, jumla wanasiasa, wanajeshi na mabingwa 280 kutoka nchi 45 watajishughulisha na mustakabali na maendeleo ya Shirika la NATO. Mada ya kwanza inahusika na hutuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani juu ya mahusiano kati ya Marekani na Ulaya. Mkutano huo utahutubiwa pia na Mawaziri wa Mambo ya Ulinzi wa Marekani na Urusi, Donald Rumsfeld na Sergei Ivanov, na kiongozi wa chama cha CDU cha Ujerumani, Bibi Angela Merkel. Maandamano kadha ya upinzani yanatazamiwa kufanyika mjini Munich. Polisi wapatao 4,000 wamewekwa kuhakikisha usalama wa mkutano huo.