1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi, aitembelea Cambodia

13 Agosti 2023

Waziri wa mambo ya kigeni wa China Wang Yi, ameitembelea Cambodia mwishoni mwa juma kutilia mkazo dhamira ya nchi yake kwa taifa hilo baada ya waziri mkuu aliyekuwa madarakani Hun Sen kumkabidhi madaraka mtoto wake.

https://p.dw.com/p/4V70x
Chinesischer FM Wang Yi besucht Kambodscha
Picha: Ouyang Kaiyu/China News Service/MAXPPP/dpa/picture alliance

Wang Yi ni kiongozi wa kwanza wa nchi za kigeni kuitembelea Cambodia tangu Hun Sen alipotangaza kuwa mwanaye ambaye pia ni mkuu wa jeshi Hun Manet mwenye miaka 45, angechukua nafasi yake.

Soma pia: Mkuu wa majeshi wa Cambodia arithi uwaziri mkuu

Msemaji wa Hun Sen, Eang Sophallet amewaambia waandishi wa habari kuwa, mkutano wake na Wang Yi unaonesha utayari wa China kushirikiana na Waziri Mkuu mteule:

Hun Sen, anayetajwa kuwa mkuu wa serikali aliyeongoza kwa muda mrefu zaidi barani Asia kupitia chama chake alishinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu baada ya kukizuia chama kikuu cha upinzani cha  the Candlelight Party kushiriki uchaguzi kwa madai ya dosari za kiufundi.  Mataifa ya magharibi na makundi ya sheria yalikosoa uchaguzi kuwa haukuwa huru wala wahaki.