1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Waziri wa mambo ya nje wa India akutana na rais wa Urusi

28 Desemba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa India Subramanyam Jaishankara, amekutana Jumatano na Rais wa Urusi Vladimir Putin wakati wa ziara yake ya siku tano nchini Urusi

https://p.dw.com/p/4adxf
Waziri wa mambo ya nje wa India Subrahmanyam Jaishankar (Kushoto) na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov ( Kulia) wahudhuria mkutano na wanahabari mjini Moscow mnamo Desemba 27, 2023
Waziri wa mambo ya nje wa India Subrahmanyam Jaishankar (Kushoto) na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov ( Kulia) Picha: Alexander Shcherbak/Tass/IMAGO

Wakati wa mkutano huo, Putin amesema kuwa uhusiano kati ya nchi hizo unaendelea vizuri hata katika nyakati za misukosuko. Putin ameongeza kuwa atamuarifu mjumbe huyo wa India kuhusu vita nchini Ukraine ambavyo waziri mkuu wake Narendra Modi amekuwa na msimamo usioegemea upande wowote kuvihusu.

Soma pia:Modi afanya mazungumzo ya simu na Putin

Taarifa kutoka ikulu ya Kremlin, imemnukuu Jaishankar akisema kuwa ni muhimu kwa mataifa hayo mawili kufanya ushirikiano endelevu wa kibiashara na kwamba mataifa hayo yanahitaji kufikiria jinsi ya kufanikisha hilo.

Soma pia: Modi amwambia Putin huu si wakati wa vita

Jaishankar pia alikutana na mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov, ambaye amesema walijadiliana kuhusu uwezekano wa ushirikiano wa kijeshi na kiufundi,  na utengenezaji wa pamoja wa aina ya silaha za kisasa.