Waziri wa mambo ya nje wa Israel azuru Bahrain
4 Septemba 2023Waziri wa mambo ya nje wa Israel Eli Cohen anazuru Bahrain kwa mazungumzo na maafisa wa vyeo vya juu, katika ziara yake ya kwanza katika mojawapo ya nchi za kiarabu katika eneo la Ghuba zenye mahusiano ya kidiplomasia na Israel.
Cohen aliwasili jana nchini Bahrain akiwa ameandamana na ujumbe wa wanasiasa na wafanyabiashara na amepangiwa kukutana na Mfalme wa Bahain pamoja na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo mjini Manama wakati wa ziara yake hiyo ya siku mbili.
Hii ni ziara ya kwanza ya Cohenkatika nchi mojawapo iliyosaini mikataba ya Abraham mnamo mwaka 2020 iliyosimamiwa na Marekani, ambayo ilishuhudia Israel ikirejesha mahusiano ya kawaida na Bahrain, Umoja wa Falme za Kiarabu na Morocco. Ziara ya Cohen inafanyika chini ya wiki mbili kabla maadhimisho ya tatu ya mikataba hiyo katikati ya mwezi huu wa Septemba.
(AFP)