Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Lammy azuru India
24 Julai 2024Waziri wa mambo ya nje ya Uingereza David Lammy ameanza juhudi za kuimarisha mchakato wa kufikia makubaliano ya biashara huru na India baada ya kuwasili mjini New Delhi katika ziara yake ya kwanza rasmi. Nchi hizo mbili zimetumia zaidi ya miaka miwili kujadiliana juu ya kile ambacho kitakuwa ni hatua kubwa kwa Uingereza huku ikitafuta masoko mbadala baada ya kujitoa kutoka kwa Umoja wa Ulaya mnamo 2020.
Soma: Waziri Mkuu wa Uingereza ziarani India
Waziri Lammy atakutana na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa India S. Jaishankar na waziri wa biashara Piyush Goyal wakati wa zaira yake ya siku mbili. Atafanya mikutano na viongozi wa mazingira na biashara kuimarisha uungwaji mkono kwa hatua za kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa, huku India ikiwa mshirika muhimu wa lazima asiyeweza kuepukika.