Kuleba yupo Beijing kwa mazungumzo ya kumaliza vita
23 Julai 2024Matangazo
China inajipambanua kama mshirika asiyegemea upande wowote katika vita hivyo na kusema haitoi usaidizi hatari kwa pande zote mbili, tofauti na Marekani na mataifa mengine ya Magharibi.
Kuleba kuelekea China kusaka suluhu ya mzozo wa Ukraine
Hata hivyo, kuongezeka kwa ushirikiano wake "usio na ukomo" na Urusi kumesababisha wanachama wa NATO kuiita China kuwa "mwezeshaji madhubuti" wa vita vya Moscow, ambavyo serikali ya Beijing haijawahi kulaani.
Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba ya hadi Ijumaa ni ya kwanza tangu vita kuanza Februari 2022.