Waziri wa uchukuzi Singapore ajiuzulu kufuatia ufisadi
18 Januari 2024Iswaran amejiuzulu wadhfa wake kufuatia mashtaka hayo dhidi yake. Katika barua iliyokuwa na tarehe ya juzi Jumanne, Iswaran amesema kwamba anayapinga mashtaka hayo na kwa sasa atajikita katika kulisafisha jina lake.
Shirika la Kuchunguza Visa vya Ufisadi nchini humo CPIB limesema waziri huyo aliyejiuzulu na ambaye alikamatwa Julai mwaka jana, anadaiwa kupokea rushwa ya zaidi ya dola laki mbili na elfu thamanini. Iwapo atahukumiwa, huenda akatozwa faini ya hadi dola laki moja za Singapore au kifungo cha miaka 7 jela.
Kisa hicho cha ufisadi ni cha nadra nchini Singapore, nchi ambayo inadai kuwa na serikali nadhifu ambayo ni nadra kuhusika na visa vya ufisadi.
Wafanyakazi wa umma Singapore wanalipwa mishahara mikubwa ili wasijihusishe na visa vya ufisadi.