1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Robert Habeck kufungua mkutano wa kibiashara Kenya

3 Desemba 2024

Waziri wa uchumi wa ujerumani Robert Habeck ameahidi kwaba Ujerumani itatowa ushirikiano wa karibu wa kiuchumi na mataifa ya Afrika kwenye mkutano wa kilele wa kibiashara kati ya nchi hiyo na bara la Afrika.

https://p.dw.com/p/4nh3o
Habeck akiwa Kenya
Waziri wa uchumi wa ujerumani Robert Habeck akiwa ziarani nchini Kenya Picha: Sebastian Gollnow/dpa/picture alliance

Akiwa mjini Nairobi, Kenya Waziri huyo wa uchumi wa Ujerumani pia ameyatolea mwito mataifa ya bara hilo kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji.Mkutano huo wa kilele unaofanyika kila baada ya miaka miwili umehudhuriwa pia na waziri mkuu wa Kenya Musalia Mudavadi. 

Takriban wajumbe 800 kutoka mataifa 35 ya Afrika  na Ujerumani wanashiriki mkutano huo  muhimu wa kibiashara kwa Ujerumani katika bara la Afrika. 

Ujerumani kufanya biashara ya nishati na Nigeria

Bara hilo ni muhimu kwa uchumi wa Ujerumani kutokana na kasi na mabadiliko yake ya kiuchumi. Bara la Afrika ni la pili kwa ukuaji wa kasi  wa kiuchumi duniani baada ya bara la Asia. 
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW