1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya waziri Westerwelle ,Uturuki na katika eneo la Ghuba.

Abdu Said Mtullya6 Januari 2010

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Westerwelle leo ameanza ziara ya siku mbili nchini Uturuki.

https://p.dw.com/p/LMdB
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle leo ameanza ziara ya siku mbili nchini Uturuki.Picha: AP

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle ,leo ameanza ziara ya Uturuki na katika nchi za Ghuba.

Suala muhimu katika mazungumzo yake na wenyeji wake wa Uturuki ni maombi ya nchi hiyo ya kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Ulaya.

Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Ulaya, ikiwa pamoja na Ujerumani, wanaunga mkono mpango wa kuipa Uturuki hadhi mahsusi na siyo uanachama kamili katika Umoja huo.

Katika ziara yake ya siku sita,waziri Westerwelle pia atazitembelea nchi za Ghuba: Saudi Arabia,Katar na Umoja wa Falme za Kiarabu. Katika ziara ya nchi hizo atakayoianza ijumaa, waziri Westerwelle anafuatana na wafanyabishara kadhaa.

Hiyo ni ziara ya pili katika nchi za kiarabu na Mashariki ya Kati. Mnamo mwezi wa Novemba mwaka jana waziri huyo alifanya ziara nchini Israel na kwenye maeneo ya Wapalestina.

Mgogoro wa Mashariki ya Kati pia utakuwa sehemu muhimu ya mazungumzo yake katika ziara ya nchi za Ghuba. Waziri huyo wa Ujerumani pia atajadili mvutano uliopo baina ya nchi za magharibi na Iran kutokana na mpango wa nyukilia wa nchi hiyo.Waziri huyo anatarajiwa kuziomba nchi hizo ziunge mkono vikwazo vinavyotarajiwa kuwekwa dhidi ya Iran.

Katika mazungumzo yake na viongozi wa nchi za Ghuba, waziri huyo wa Ujerumani pia atajadili suala la harakati za kupambana na ugaidi duniani na hasa matukio ya hivi karibuni nchini Yemen

Leo bwana Westerwelle anatarajiwa kuwa na mazunguzo na waziri mwenza wa Uturuki, Ahmet Dovutoglu. Pia atakutana na waziri mkuu Erdogan. Waziri Westerwelle amesifu juhudi za kuleta mageuzi nchini Uturuki,lakini amesema hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa.

Mwandishi/ Bettina Max/ZA/DPA

Imetafsiriwa na Mtullya Abdu

Mhariri: Othman, Miraji