1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa watinga fainali soka la wanaume Olimpiki

Sylvia Mwehozi
6 Agosti 2024

Na katika soka wenyeji Ufaransa watacheza fainali ya Olimpiki kwa wanaume kwa mara ya kwanza baada ya miaka 40 baada ya kuwalaza Misri 3-1 katika muda wa ziada.

https://p.dw.com/p/4j8xP
Uwanja wa Parc des Princes
Uwanja wa Parc des Princes unaotumika kwa mchezo wa soka katika OlimpikiPicha: Christophe Ena/AP/picture alliance

Wenyeji Ufaransa watacheza fainali ya Olimpiki kwa wanaume kwa mara ya kwanza baada ya miaka 40 baada ya kuwalaza Misri 3-1 katika muda wa ziada katika uwanja wa Lyon siku ya Jumatatu na watamenyana na Uhispania kuwania medali ya dhahabu. Uhispania wameifunga Morocco mabao 2-1.

Misri, ambao walikuwa wakicheza nusu fainali yao ya tatu ya Olimpiki, walipata mikwaju mingi zaidi kwenye lango katika kipindi cha kwanza. Upande wa mpira wa kikapu Uholanzi imeshinda medali ya dhahabu katika mchezo wa mpira wa kikapu wa 3x3 kwa wanaume kwa kuitandika Ufaransa katika muda wa nyongeza.Mwanariadha wa kasi zaidi duniani ni Mmarekani Lyles

Timu ya wanawake ya Ujerumani imetwaa medali ya dhahabu katika mpira wa kikapu kwa kuichapa Uhispania. Hiyo ni medali ya kwanza kabisa ya Olimpiki ya Ujerumani katika mpira wa kikapu. Marekani ambayo ilishinda Olimpiki ya Tokyo mwaka 2020 iliwacharaza Canada na kubeba medali ya shaba.