1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaMalawi

WHO: Kipindupindu kimeuwa zaidi ya watu 1,200 Malawi

10 Februari 2023

Watu 1, 210 wamefariki nchini Malawi kutokana na mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu tangu Machi 2022.

https://p.dw.com/p/4NK2A
Mikroskopaufnahme von Cholera Bakterien
Picha: CAVALLINI JAMES/BSIP/picture alliance

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema kipindipindu kimesababisha vifo vya takribani 1,210 huku suala la chanjo likipewa nafasi ndogo na mataifa mengine kadhaa yakitoa ripoti ya mripuko huo.

Visa vilivyothibitishwa tayari vimeripotiwa kuvuka mpaka wa Msumbiji, wakati WHO ikisema imetathmini hatari ya sasa ya kuenea ndani ya Malawi na katika nchi nyingine jirani kuwa juu sana.

Taarifa ya sasa ya shirika hilo inasema maambukizi hivi sasa yanaendelea katika wilaya 27 kati ya 29 za Malawi, huku nchi hiyo ikishuhudia ongezeko la asilimia 143 la wagonjwa mwezi uliopita ikilinganishwa na Disemba.