1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

WHO: Kitisho cha njaa bado kingalipo katika Ukanda wa Gaza

3 Mei 2024

Shirika la Kimataifa la Afya, WHO limetahadharisha juu ya kitisho cha njaa kinachoendelea kwenye Ukanda wa Gaza ulioahiribiwa vibaya na vita kati ya Hamas na Israel.

https://p.dw.com/p/4fUSe
WHO I Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus Picha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

WHO imeripoti kwamba zaidi ya watoto 40 wa chini ya miaka mitano na wenye utapiamlo mkali wamefikishwa hospitali katika Ukanda wa Gaza wakiwa na matatizo zaidi ya kiafya tangu mwezi Machi.

Baadhi ya watoto wa miaka miwili walikuwa na kilogram 4 tu, tofauti na wastani wa kilo 10 hadi 12. 

WHO: Gaza bado inakabiliwa na kitisho cha njaa

Daktari mwandamizi wa WHO huko Gaza, Ahmed Dahir, amewaambia waandishi habari mjini Geneva kupitia video kwamba hali ya ufikishwaji wa chakula bado ni mbaya na kwa maana hiyo hawezi kuepuka kuzungumzia kitisho cha njaa kwa sasa.