WHO: Maambukizi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu yaongezeka duniani
28 Oktoba 2022Ripoti mpya ya Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, inasema dadi ya watu walioambukizwa ugonjwa wa kifua kikuu, ikiwa ni pamoja na uwepo wa wenye kupata usugu wa dawa, imeongezeka kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa. Shirika hilo limesema kwa mwaka 2021 zaidi ya watu milioni 10 duniani kote wamefikwa na maradhi ya kifua kikuu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.5 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Ripoti inasema takribani watu milioni 1.6 wamekufa. WHO inasema kiasi ya visa 450,000 vimehusishwa na usugu wa madawa ya ugonjwa huo, ikiwa ni ongezeko la asilimia 3, kwa ulinganifu wa mwaka 2020. Janga la Covid-19 limevuruga huduma kwa watu wenye ugonjwa wa kifua kikuu, ikiwa sawa na progamu nyingine. Shirika hilo limesema watu wengi walishindwa kugunduliwa, jambo ambalo limesababisha idadi ya maambukizi mapya yaligunduliwa kupungua kutoka watu milioni 7 kwa 2019 hadi milioni 2020.
Visa vingi vya maambukizi vimetokea India, Indonesia, Myanmar na Ufilipino
Mkurugenzi anaehusika na mpango maalum wa dharura kwa Kifua Kikuu katika shirika hilo, Tereza Kasaeva amesema kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili WHO inatoa taarifa ya kuongezeka kwa waginjwa na kadhali kujitokeza kwa hali ya usugu kwa baadhi ya waginjwa.
"Ugonjwa wa kifua kikoo unatokea katika kila sehemu ya duniani. Kwa mwaka 2021 mzigo mgubwa wa ugonjwa huo kwa WHO ulikuwa kusini-mashariki mwa kanda ya Asia, kwa asilimia 46, ukifuatiwa na WHO kanda ya Afrika asilimia 23, na WHO eneo la Magharibi mwa Pasifiki kwa aslimia 18." alisema Tereza.
Miaka ya 2009 hadi 2019 ilikuwa ya unafuu kwa ugonjwa wa Kifua Kikuu.
Kwa zingatio la ripoti hii ya sasa taarifa ya kila mwaka inakadiria idadi ya waliokuwa wanapoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Kifua Kikuu ilipungua zaidi katika kipindi cha miaka ya 2005 na 2019, lakini makadirio ya ya 2020 yanaonesha hali imekua tofauti. Na idadi kubwa ya vifo imeripotiwa zaidi katika mataifa manne ambayo ni India, Indonesia, Myanmar na Ufilipino.
Soma zaidi:Bado kuna changamoto ya kuudhibiti Ugonjwa wa kifua kikuu
Lakini kwa ujumla mataifa manane ambayo yanafanya zaidi ya theluthi mbili vifo vyote duniani ni pamoja na hayo manne ya awali ni China, Pakistan, Nigeria, Bangladesh na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Ripoti hiyo ya sasa ya WHO inaonya endapo hakutakuwa na hatua madhubuti ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa mara nyingine unaweza kuwa chanzo kikuu cha vifo vyote vinavyotokea dunia ukichukua nafasi ya Covid-19
Chanzo: AP/ AFP