1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yaidhinisha chanjo ya Bavarian Nordic dhidi ya Mpox

14 Oktoba 2024

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, limesema limeidhinisha chanjo ya mpox ya Bavarian Nordic kuwachanja vijana wenye umri wa miaka 12 hadi 17, umri unaozingatiwa kuwa katika hatari zaidi ya milipuko ya ugonjwa huo.

https://p.dw.com/p/4llf4
DR Kongo | Kuanza kwa utoaji wa chanjo ya mpox katika eneo la Kamanyola
Kuanza kwa utoaji wa chanjo ya mpox katika eneo la Kamanyola, DR KongoPicha: Ernest Muhero/DW

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, limesema limeidhinisha chanjo ya mpox ya Bavarian Nordic kuwachanja vijana wenye umri wa miaka 12 hadi 17, umri unaozingatiwa kuwa katika hatari zaidi ya milipuko ya ugonjwa huo.

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, WHO imesema ilitoa idhini ya vijana kupokea chanjo hiyo mnamo Octoba 8, baada ya Umoja wa Ulaya kuiidhinisha chanjo hiyo kwa vijana mnamo Septemba.

Soma pia: WHO: Chanjo za mpox kuwasili hivi karibuni nchini DRC

Chanjo nyingine ya mpox, LC16, iliyotengenezwa na kampuni ya Japani ya KM Biologics , inaweza tayari kutolewa kwa watoto, kulingana na shirika la udhibiti la Japan, ingawa inahitaji aina maalum ya
sindano.

WHO ilitangaza mpox kuwa dharura ya afya ya umma duniani kwa mara ya pili katika miaka miwili mwezi Agosti baada ya aina mpya ya virusi hivyo kusambaa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hadi nchi jirani.