MigogoroMamlaka ya Palestina
Watu zaidi ya 44,000 wauawa katika Ukanda wa Gaza
15 Desemba 2024Matangazo
Idadi hiyo inajumuisha vifo 46 vilivyotokea masaa 24 yaliyopita, imesema wizara hiyo.
Aidha watu 106,759 wamejeruhiwa kwenye Ukanda huo tangu kuzuka kwa vita hivyo, baada ya wanamgambo hao kuishambulia Israel, Oktoba 7, 2023.
Vita hivyo aidha vimesababisha idadi kubwa ya watu milioni 2.4 wa Gaza kuyakimbia makazi yao, na wengine wakikimbia zaidi ya mara moja.
Jeshi la Israel limekuwa likifanya mashambulizi makubwa kaskazini mwa Gaza kwa wiki kadhaa sasa, likisema linalenga kuzuia wanamgambo wa Hamas kujiunda upya.