1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wolsburg na Leverkusen wawania kufanya vizuri

30 Oktoba 2015

Timu mbili zinazoshiriki katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya Wolfsburg na Bayer Leverkusen zitaoneshana kazi leo Jumamosi na Borussia Dortmund inawania kujiimarisha katika nafasi ya pili.

https://p.dw.com/p/1GxIV
Fußball Bundesliga 10. Spieltag SV Darmstadt 98 gegen VfL Wolfsburg
Wachezaji wa Wolfsburg wakishangiria baoPicha: picture-alliance/dpa/F. von Erichsen

Schalke 04 inawania kuwaonesha mashabiki wake kwamba bado inaweza kushikilia nafasi ya kucheza katika Champions League , wakati ikiwasubiri Ingolstadt leo jioni 31.10.2015).

Deutschland Bundesliga Fabian Johnson Borussia Mönchengladbach
Fabian Johnson wa Borussia MoenchengladbachPicha: picture-alliance/dpa/Revierfoto

Makamu bingwa wa Bundesliga VFL Wolfsburg wanawasubiri Bayer Leverkusen iliyoshika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi msimu uliopita katika pambano kubwa la mchezo wa 11 wa Bundesliga.

Karatasini pambano hilo ni la wababe na vigogo wa Bundesliga kama inavoonekana pia katika nafasi zao kwa sasa katika ligi hiyo , licha ya kwamba timu hizo zote hazifurahishwi na nafasi walizonazo pamoja na idadi ya pointi zao. Nafasi zao zinapaswa kuwa juu zaidi.

Dieter Hecking
Kocha Dieter Hecking wa WolfsburgPicha: picture-alliance/dpa/A. Gebert

Kwa sasa Wolfsburg inashikilia nafasi ya nne wakati Leverkusen iko katika nafasi ya sita. Lakini timu hizo zinapishana kwa pointi moja tu , hali ambayo inaonesha kupungukiwa na nguvu zake za msimu uliopita.

Kocha wa VFL Wolfsburg Dieter Hecking anafafanua zaidi kuhusu hali ya timu yake ilivyo.

"Ni lazima tukubali kushindwa na tunafahamu dhidi ya nani tulishindwa. Kwa tulivyocheza katika kipindi cha kwanza kila mmoja ameona. Hatukuwa na jibu. Nilitaraji timu yangu ingeonesha upinzani zaidi, lakini hayo yamepita na lazima sasa tuangalie mbele na ni lazima tutambue kwamba mpambano wa leo dhidi ya Leverkusen tutajaribu tena kuweka msingi katika ligi, kwamba tuko katika kiwango cha kutoa ushindani na hii ndio kazi tunayopaswa kuifanya Jumamosi jioni."

Fußball DFB-Pokal BVB Borussia Dortmund vs. SC Paderborn
Wachezaji wa Borussia Dortmund wakishangiria baoPicha: Getty Images/Bongarts/C. Koepsel

Kitu gani kimezibadilisha Hertha Berlin na Borussia Moenchengladbach katika muda wa wiki chache zilizopita. Hili ni swali linaloulizwa na mashabiki na wachambuzi wa masuala ya soka hapa Ujerumani. Mashabiki wa Hertha Berlin hawakuwa na hakika vipi timu yao itakavyoweza kufanya msimu huu baada ya kuponea chupu chupu kushuka daraja. Lakini wanaogelea hivi sasa katika mafanikio ya kushangaza wakati kocha Pal Dardai ameiongoza timu hiy<o kutoka mji mkuu kwenda hadi nafasi ya tano ya msimamo wa ligi baada ya michezo 10.

Hertha inakumbana na Borussia Moenchengladbach ambayo nayo imeonesha makali baada ya kushindwa katika michezo mitano ya mwanzo na kumlazimisha kocha wao Lucien Favre kujiuzulu.

Andre Schubert alichukua hatamu za timu hiyo kama kocha wa mpito na kupata ushindi mara tano mfululizo , hali ambayo imeirusha Gladbach hadi nafasi ya saba na kuwasukuma wapenzi wa timu hiyo kudai kwamba apewa kazi hiyo rasmi.

Taji laelekea kwenda Munich

Wakati taji la Bundesliga linaonekana kuelekea Munich kwa Bayern macho yamegeukia sasa mpambano wa kuwania nafasi ya Champions League na ligi ya Ulaya. Ushindi kwa Hertha unaweza kuisukuma timu hiyo kuingia katika nafasi nne za juu.

Borussia Mönchengladbach Trainer Andre Schubert
Kocha wa Borussia Moenchengladbach, Andre SchubertPicha: Getty Images/Bongarts/M. Hangst

Schalke inayoshikilia nafasi ya tatu katika msimamo wa sasa inaikaribisha Ingolstadt. Borussia Dortmund inajisikia mara hii kuelekea kucheza katika Champions League baada ya kikosi cha kocha mpya Thomas Tuchel kuwa katika kiwango cha juu mara hii. Dortmund inasafiri kwenda Bremen kupambana na Werder Bremen jioni ya leo.

Michezo ya Jumapili ni kati ya VFB Stuzttgart dhidi ya Darmstadt , wakati Hannover 96 , ikiwa na pointi moja tu kuliko Stuttgart inakwenda kwa SV Hamburg.

Mwandishi : Kops, Calle / Sekione Kitojo / dpae

Mhariri: Yusuf Saumu