SiasaChina
Xi: China ´isichafuliwe jina´ kutokana na mzozo wa Ukraine
7 Mei 2024Matangazo
Xi aliye ziarani nchini Ufaransa amewaambia waandishi habari akiwa na mwenyeji wake rais Emmanuel Macron, kwamba China inapinga kutumiwa mzozo wa Ukraine kama karata ya kuilaumu na kuchochea enzi mpya ya vita baridi.
Amesema China haijabikia kuwa mtizamaji na badala yake inafanya jitihada za kufanikisha kupatikana amani. Mbali ya mzozo wa Ukraine, rais Xi pia ametumia ziara yake ya Ufaransa kujadili masuala ya biashara na Ufaransa pamoja na kanda nzima ya Ulaya.
Hii leo Jumanne, Xi atasafiri na rais Macron kwenda jimbo la milimani la Pyrenees kabla ya kuelekea Hungary na Serbia kuendelea na ziara yake barani Ulaya.