1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Xi Jinping akutana na Sullivan Beijing

29 Agosti 2024

Rais wa China Xi Jinping leo amekutana na mshauri wa Usalama wa Marekani, Jake Sullivan mjini Beijing.

https://p.dw.com/p/4k33Z
China | US Sicherheitsberater Jake Sullivan trifft Xi Jinping in Peking
Picha: Trevor Hunnicutt/Pool Photo/AP/picture alliance

Mapema leo Sullivan alikutana na afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la China, Jenerali Zhang Youxia, huku nchi hizo mbili zikiimarisha uhusiano wao katika juhudi za kuzuia tofauti katika Bahari ya China Kusini na Taiwan zisizidi na kuwa mzozo kamili.

Katika ziara yake ya siku tatu, Sullivan amekutana pia na Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China, na afisa mkuu wa sera za kigeni wa chama tawala cha Kikomunisti.

Jana, Ikulu ya Marekani ilisema nchi zote zinapanga mazungumzo kwa njia ya simu kati ya Rais Xi na Rais Joe Biden, katika wiki zijazo.

Ziara ya Sullivan nchini China, ina lengo la kuleta utulivu wa uhusiano baina ya nchi hizo mbili ili kuepusha migogoro.