1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyomsibu mkuu wa shirika la IMF magazetini

16 Mei 2011

Kisa cha kukamatwa mwenyekiti wa shirika la fedha la kimataifa na mkutano mkuu wa chama cha FDP mjini Rostock ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa zaidi hii leo

https://p.dw.com/p/11GmY
Dominique Strauss-Kahn amekamatwaPicha: picture alliance/dpa



Tuanzie lkini na kisa cha Dominique Strauss-Kahn.Gazeti la Saarbrücker Zeitung linaandika:

Mkuu wa shirika la fedha la kimataifa na mgombea anaepewa nafasi nzuri ya kushinda uchaguzi wa rais mwakani nchini Ufaransa-amewekwa korokoroni kwa tuhuma za ubakaji.Hakuna zilzala kubwa zaidi ya hiyo iliyoteketeza hadhi tangu ya kisiasa mpaka ya kiutu ya Dominique Strauss-Kahn.Bila ya shaka lazma kwanza watu wasimmwagie matope mwanasiasa huyo mashuhuri wa Ufaransa kabla ya kwanza makosa anayotupiwa kubainika.Lakini pekee ile jinsi alivyokmatwa na fadhaa ya maelezo yaliyofuatia yamesha mtia dowa.Kwa namna hiyo wadhifa wake katika taasisi ya fedha ya kimataifa na nafasi yake katika chama cha kisoshialisti cha Ufaransa,mtu anaweza kusema ni mbio za sakafuni.


Gazeti la Nürnberger Nachrichten linahisi DSK,kama Dominique Strauss-Kah nanavyojulikana nchini Ufaransa,ana kila sifa ambazo wenghi wa wapinzani wake wanazimezeya mate.Gazeti linaendelea kuandika.

Strauss-Kahn ana kipaji katika masuala ya kiuchumi ,ana moyo wa kijamaa na wakati huo huo ana hadhi ya kuweza kuwa rais-sifa ambazo wengi katika utawala wa Sarkozy wanazimezea mate.Kwa hivyo,wale wanaohisi kwamba wanasiasa wote kwa jumla hawaaminiki,watapata kichwa.Nao ni wale wanaoelemea kwa mikururo upande wa chama cha Marine Le Pen,Front National.

FDP Parteivorsitzende Philipp Rösler hält beim Bundesparteitag der FDP in Rostock seine Hauptrede
Mwenyekiti mpya wa chama cha FDP,Philipp RöslerPicha: picture-alliance/dpa


Mada yetu ya pili magazetini inahusu mkutano mkuu wa chama cha kiliberali cha FDP uliomalizika jana mjini Rostock.Gazeti la Landeszeitung la mjini Lüneburg linaandika:

"Si porojo,ilikuwa hotuba ya dhati aliyoitoa mwenyekiti mpya wa FDP,Philipp Rösler kwa muda wa dakika 70 na kuwapandisha jazba wajumbe katika mkutano huo mkuu mjini Rostock.Rösler ameahidi mageuzi na kuachana na sifa ya chama kinachojishughulisha na mada moja tuu ya kodi ya mapato.Suala lakini ni kama hayo yatasaidia kuondokana na mkosi wa asili mia tatu za maoni ya waapiga kura,hali hiyo itabainika baada ya wiki kadhaa kupita.

Deutschland Musik ESC 2011 Eurovision Song Contest Finale Aserbaidschan Ell/Nikki gewonnen
Washindi wa shindano la nyimbo-Eúrovision wanatokea AzerbaidjanPicha: dapd


Mada yetu ya mwisho inahusu shindano la wimbo bora barani Ulaya-Eurovision mjini Düsseldorf.Gazeti la Volksstimme la mjini Magdeburg linaandika:

Shindano la wimbo bora barani Ulaya limefana.Lini mtazamaji televisheni aliwahi kujionea uwanja wa mpira ukigeuka jukwaa la burudani?Na wasanii jee?Ndio watu wameimba pia.Mtazamaji anatambua hivi sasa makundi ya wanamuziki wa kiume yameenea barani Ulaya sawa na mchanga baharini.Na Mwanamuzik wa jazz kutoka Italy alikuwa nusra ashinde.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Abdul-Rahman,Mohammed