Maombi zaidi ya milioni 1 ya hifadhi yalirekodiwa Ulaya 2023
28 Februari 2024Matangazo
Idadi ya waomba hifadhi barani Ulaya mwaka uliopita ilizidi milioni moja. Hayo ni kulingana na shirika la waomba hifadhi la Umoja wa Ulaya lenye makao yake makuu katika kisiwa cha Malta.
Kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka iliyotolewa leo mjini Valleta, shirika hilo lilirekodi jumla ya maombi milioni 1.14 katika mataifa 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya.
Soma: Umoja wa Ulaya watahahdharisha wimbi la wakimbizi kutoka Sudan
Ikilinganishwa na mwaka uliopita, hilo ni ongezeko la asilimia 18 ya waomba hifadhi. Wengi walikimbia machafuko nchini Syria na Afghanistan.
Ujerumani ilisalia kuwa nchi inayopendelewa na wengi, ambapo maombo mapya 334,000 ya hifadhi yaliwasilishwa kati ya Januari na Disemba 2023.