JamiiMalawi
Zaidi ya nusu ya watoto wanakabiliwa na utapiamlo Malawi
7 Machi 2023Matangazo
Makadirio ya shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia watoto, UNICEF yameonyesha kuwa watoto wapatao milioni 4.8, sawa na nusu ya watoto wote katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, wanahitaji msaada wa kiutu.
Ripoti ya shirika hilo imesema kua hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Machi, inatarajiwa kuwa watoto zaidi ya 213,000 watakumbwa na utapiamlo mkubwa, 62,000 miongoni mwao wakiweka katika kundi lenye tatizo lililopitiliza.
Afisa Mkazi wa UNICEF nchini Malawi, Rudolf Schwenk, amesema mtoto anayesumbuliwa na utapiamlo yuko hatarini kufa kutokana na kipindupindu, mara 11 zaidi ya mtoto mwenye afya njema.
Umoja wa Mataifa umeomba kiasi cha dola milioni 50 za kukabiliana na mripuko wa kipindupindu nchini Malawi.