1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya raia 150 wauawa Kongo katika wiki mbili: UN

19 Aprili 2023

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa jana imesema kuwa watu zaidi ya 150 wameuawa katika mkoa wa Ituri kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndani ya wiki mbili zilizopita kutokana na mashambulizi

https://p.dw.com/p/4QIBV
Milizsoldaten bewaffnete Gruppe URDPC/CODECO
Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini imekumbwa na vurugu zinazozidi kuongezeka, zinazofanywa na makundi ya wanamgambo yenye silaha katika eneo hilo lenye utajiri wa madini linalopakana na Uganda.

Kundi mojawapo, CODECO linadai linawalinda watu wa jamii ya Walendu, kutoka jamii nyingine ya Wahema pamoja na jeshi la serikali.

Soma pia: Kuna jumla ya makundi 266 yanayomiliki silaha mashariki ya Kongo

Wahema wenyewe wana kundi lao la wanamgambo lijulikanalo kama Zaire, katika eneo hilo ambalo pia linapatikana kundi la ADF lenye mafungamano na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu, IS.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu msaada wa kiutu, OCHA limeonya kuwa mashambulizi yasiyokoma katika wilaya za Djugu, Irumu na Mambasa yamegharimu maisha ya watu zaidi ya 150 tangu kuanza kwa mwezi Aprili.