Wanamgambo wawaua zaidi ya raia 45, Ituri
13 Juni 2023Matangazo
Msemaji wa jeshi katika jimbo la Ituri Jules Ngongo Tshikudi amesema mashambulizi hayo ambayo pia yamesababisha wengine 10 kujeruhiwa kuwa ni "kitendo cha hujuma" dhidi ya majaribio ya kurejesha amani na kusema uchunguzi unaendelea.
Taarifa ya MONUSCO imelitaja kundi la waasi wa CODECO, ambalo limetapakaa katika eneo hilo tete la mashariki kuwa linahusika na mauwaji hayo katika kambi iitwayo "LALA".
CODECO ni kundi ambalo linajinasibu kulinda maslahi ya jamii ya wakulima ya Lendu. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa wapiganaji wake wamewaua mamia ya raia katika eno la Ituri na kuwalizimisha maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao.